Volkswagen kuikabili Mercedes F1

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Kampuni ya magari ya Volkswagen

Kampuni ya Volkswagen ya pili kwa utengenezaji magari duniani, inafanya upembuzi yakinifu kuhusu kuingiza magari yake katika michezo ya Formula 1.

Vyanzo vya habari vinasema uchambuzi huo unafanywa na mkuu wa zamani wa timu ya Ferrari Stefano Domenicali, ambaye alikodishwa na kampuni ya magari ya Audi ya VW mapema mwaka huu.

Hamu yake imechochewa na mafanikio ya kampuni pinzani ya Mercedes, ambayo ni mabingwa wapya wa mbio za magari ya langa langa ya Formula 1

Lakini uamuzi wa kujiunga na F1 kutategemea mabadiliko ya uongozi katika kampuni ya VW au F1.

Ferdinand Piech, mkuu wa bodi ya usimamizi wa makampuni ya VW, na mkuu wa matngazo wa F1 Bernie Ecclestone wamekuwa katika uhusiano mbaya kwa muda mrefu.

Angalau mmoja wao atatakiwa kuondoka katika vyeo vyao vya sasa kabla ya kampuni ya VW kuingia katika F1.