Mutharika ajinyima nyongeza ya mshahara

Rais Peter Mutahrika wa Malawi Haki miliki ya picha BBC World Service

Rais Peter Mutharika wa Malawi na naibu wake wameakhirisha kujipa nyongeza ya mishahara baada ya kuzuka malalamiko.

Nyongeza kutoka mshahara wa dola 3,000 na kufikia dola 5,000 kila mwezi, imezusha malalamiko nchini Malawi ambako pato la nusu ya wananchi halitimii dola moja kwa siku.

Bwana Mutharika na makamo wake, Saulos Chilima wamesema hawatojipa nyongeza ya mishahara hadi uchumi wa nchi utengenee.

Kabla ya viongozi hao kushika madaraka wafadhili walisimamisha msaada wa dola 150-milioni kwa sababu ya wasiwasi kuhusu rushwa.

Mishahara ya wabunge itazidishwa asili-mia-mia-tatu (300%)