Marekani yazungumzia operesheni zake

Image caption Waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuck Hagel

Marekani imesema hakutakuwa na mabadiliko katika operesheni zake kwa ajili ya kuachiliwa huru raia wake waliokamatwa mateka.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuck Hagel amesema hakutakuwa na mabadiliko yoyote katika operesheni hizo kwa ajili ya kuachiliwa huru Wamarekani wanaoshikiliwa mateka na makundi ya wapiganaji, Licha ya kushindwa kwao katika siku za hivi karibuni.

Hagel ametetea jaribio la uokoaji lililofanywa hivi karibuni na kikosi maalum, ambapo mwandishi wa Kimarekani Luke Somes na Mwalimu raia wa Afrika kusini Pierre Korkie waliuawa na wanamgambo wa Al Qaeda nchini Yemen.

Awali Kikosi maalumu cha jeshi la Marekani kilishindwa katika operesheni iliyofanya kumuokoa raia wake huyo na pia katika kuachiliwa kwa mwandishi mwingine wa habari James Foley Julai mwaka huu nchini Syria, ambaye alikuwa akishikiliwa na wapiganaji wa Islamic State na baadaye kuchinjwa.