Wafungwa wengi watoroshwa Nigeria

Gereza iliyovamiwa na Boko haram siku za nyuma Haki miliki ya picha

Watu waliokuwa na silaha wamevamia gereza katika mji wa Minna, katikati mwa Nigeria, na kuwaachilia huru wafungwa 200.

Walingia kwa nguvu kwenye jela Jumamosi katika jimbo la Niger.

Polisi wanasema haijulikani ikiwa uvamizi huo ulifanywa na kundi la wapiganaji Waislamu, Boko Haram, au gengi la wahalifu.

Boko Haram wamevamia magereza kadha katika miaka ya karibuni.