Mbunge anaswa akicheza kikaoni

Image caption Mchezo wa simu Candy Crash

Mbunge wa chama tawala cha Conservative nchini Uingereza , amekiri kucheza mchezo maarufu kwenye tabiti yake wakati wa kikao cha kamati moja la bunge hilo.

Jarida la The Sun, limechapisha picha za mbunge huyo kwa jina Nigel Mills akicheza Candy Crush Saga kwenye tabiti yake, wakati wa mkutano wa kamati hio kuhusu mageuzi ya sera ya serikali kuhusu malipo ya uzeeni.

Jarida hilo linasema Bwana Nigel alicheza mchezo huo kwa zaidi ya saa mbili.

Hata hivyo amejitetea akisema alifahamu kilichokuwa kinaendelea katika kamati hiyo na kwamba lihusika katika kuuliza maswali. Hata hivyo alikiri kucheza mara mbili na kusema atajaribu kujizuia kucheza mchezo huo katika siku za usoni akiwa kazini.