Wahamiaji sharti waongee kijerumani nyumbani

Image caption Wahamiaji wanaosajiliwa kuingia Ujerumani

Wahamiaji wanaokimbilia Ujerumani wanashurutishwa kuzungumza kijerumani sio tu katika maeneo ya umma bali pia katika nyumba zao.

Sharti hili limetolewa na chama tawala cha Bavaria na kuzua hasira miongoni mwa watu wengi nchini humo.

Chama cha Christian Social Union (CSU), mshirika wa Chansela Angela Merkel, kinasema kuwa hoja hio ni jambo la kujadiliwa wala sio kwamba eti ni sera rasmi ya serikali.

Wakosoaji wa pendekezo hilo tayari wameelezea gadhabu kwenye mtandao wa Twitter

Baadhi ya watu wameelezea mshangao wao kuhusu siasa za nchi kuelekezwa majumbani mwa watu.

Pendekezo hilo linasema kuwa watu wanaotaka kuendelea kuishi nchini humo kudumu, wanapaswa kuzungumza kijerumani katika maeneo ya umma na hata nyumbani.

Katibu mkuu wa chama hicho, CSU, Andreas Scheuer anasema pendekezo hilo limeandaliwa vyema na kwamba linaungwa mkono na wengi.

Baadhi ya wanasiasa wanasema itakuwa vigumu kutekeleza penedezko hilo ikiwa litapistishwa kuwa sera wakisema polisi ndio watahitajika kutembea katika majumba ya watu kuhakikisha kuwa hilo linatekelezwa.

Hata hivyo wanasiasa wengine waliounga mkono pendekzo hilo wanasema halina msingi wa kisiasa

Wanaopinga pendekzo hilo wanasema kilichosalia ni kwa wanasiasa waliopendekeza hilo kuwashurutisha watu kuwa na mazulia yenye rangi nyeupe na nyekundu majumbani mwao.

Ajenda ya chama cha CSU imekuwa ikilenga sana maswala ya uhamiaji.