Ukatili wa majasusi Marekani wafichuliwa

Image caption Mojawapo ya mbinu zinazotumiwa na CIA kuwatesha washukiwa

Ripoti ya Seneti Marekani imekosoa vikali zinazotumiwa na CIA, kuwahoji washukiwa wa uhalifu, kwamba ni za kikatili na zisizofaa.

Ripoti ya kamati ya bunge la Seneti nchini Marekani imekosoa vikali mbinu zinazotumiwa na Shirika la Ujasusi la nchi hiyo za kuwahoji washukiwa wa uhalifu na kuelezea kwamba ni za kikatili na zisizofaa.

Mwenyekiti wa kamati ya usalama ya bunge la seneti Dianne Feinstein amesema katika baadhi ya matukio wanavyotendewa washukiwa hao ni sawa na mateso.

''Watu waliowekwa kizuizini walipaswa kutii mbinu zilizokuwa zikitumiwa, kuvuliwa nguo na kuachwa watupu, walikuwa wakiwekwa katika hali ya mateso ya muda mrefu.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Shirika la Ujasusi la marekani, CIA tuhumani

Walikuwa wakizuiwa kulala kwa siku kadhaa, hadi saa 180- ikiwa ni sawa na siku saba na nusu, zaidi ya wiki bila ya kulala, kawaida wakiwa wamwesimama au katika hali ya kuwachosha na wakati huohuo mikono yao ikiwa imefungwa pamoja juuya vichwa.

Mbonu hizo za utesaji zilianzishwa baada ya shambulio la kigaidi la Septemba 11, mwaka 2001 nchini Marekani...''

Mbinu hizo zinazotumiwa na shirika hilo la ujasusi zimeelezwa na wabunge hao wa seneti kuwa zinamapungufu na kwamba CIA imekuwa ikitoa taarifa zisizo sahihi kwa umma.