Wakimbizi wa Syria wanahangaika sana

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakimbizi wa Syria

Shirika la Umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi linaloungwa mkono na mashirika zaidi ya 30 ya kibinaadamu, limeyaomba mataifa yote duninai kuwakubali wakimbizi zaidi walioathirika na vita vya kiraia nchini mwao.

Shirika hilo la UNHCR limeandaa mkutano leo mjini Geneva ambapo nchi tajiri kutoka eneo nje ya eneo hilo zitaombwa kuwapokea angalau wakimbizi laki moja na elfu 30.

Zaidi ya watu milioni tatu wamekimbia Syria karibu wote wakiwa wanaishi katika kambi za wakimbizi katika mataifa jirani.

Mpaka sasa ni maefu kidogo ya wakimbizi waliopata hifadhi Ulaya au Marekani.

Wito huo kwa nchi tajiri kukubali asilimia 5 ya wakimbizi hao ina maana kuwapokea wakimbizi laki moja na elfu 80 wanawake na watoto au watoto walio peke yao wakiwa ndio wengi wa walio katika hatari kufikia mwisho wa mwaka ujao.

Lakini serikali nyingi na Umoja a mataifa zinaona kama kuwapa makaazi mapya wakimbizi hao kuwa hatua ya mwisho isiyo bora- inadhaniwa kwamba kila wakimbizi wakiwa karibu na nyumbani basi ndipo kunapokuwa na uwezekano wao kurudi.