Pistorius:Kiongozi wa mashitaka akata rufaa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Oscar Pistorius

Jaji mmoja nchini Afrika Kusini, ameahirisha uamuzi wake ikiwa ataruhusu mwendesha mashtaka kukata rufaa dhidi ya hukumu ya Pistorius

Jaji huyo Thokozile Masipa, aliahirisha kesi hiyo hadi siku ya Jumatano, akisema anataka muda zaidi kuchunguza tetesi zilizowasilishwa mahakamani na upande wa mashitaka ukitaka mahakama imuongfeze adhabu Pistorius.

Mwendesha mashtaka Gerrie Nel aliiambia mahakama hiyo kuwa hukumu hiyo aliyopewa Pistorius ni ndogo sana.

Oscar Pistorius huenda akaachiliwa huru kutoka gerezani baada ya miezi kumi tu huku akitarajiwa kutumikia kifungo kilichosalia nyumbani.

Alifungwa jela miaka mitano mwezi Oktoba kwa kosa la mauaji bila ya kukusudia na siku ya Jumatano mwendesha mashitaka atafahamu ikiwa anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu ya Pistorius au la.

Pistorius alijipata matatani baada ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp, mwaka jana.

Kiongozi wa mashitaka pia anataka kupinga hukumu ya mauaji dhidi ya Pistorius.

Pistorius mwenye ulemavu wa miguu aliondolewa kosa la mauaji kwa kukusudia. Hata hivyo mawakili wake wamepinga rufaa hio iliyowasilishwa na kiongozi wa mashitaka wakisema adhabu hiyo inamtosha Pistorius.