Watanzania waadhimisha miaka 53 ya uhuru

Image caption Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere

Tanzania bara leo inaadhimisha miaka 53 toka ilipojipatia uhuru toka kwa Muingereza Desemba 9, mwaka 1961.

Maadhimisho haya ya 53 ni muhimu kwa Watanzania, kutokana na kwamba nchi ipo katika kipindi cha uchaguzi, ambapo Watanzania siku ya Jumapili Desemba 14, watapiga kura, katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji.

Uchaguzi huo ni muhimu, kutokana na viongozi katika ngazi hiyo kuwa karibu kabisa na jamii.

Tanzania pia inaadhimisha miaka 53 ya uhuru wake ikiwa katika harakati za uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Ni miaka 53 tangu Tanzania ijipatie uhuru wake, lakini hali za Watanzania wengi bado ni duni, kiuchumi na kijamii.