'Dawa' ya mpango wa uzazi kwa wanaume

Image caption Mmea wa Gendarusa ambao unasemekana kuzuia wanaume kuzaa

Wanasayansi wanadai kuwa dawa mpya iliyozinduliwa ya mpango wa uzazi kwa wanaume imefanikiwa kwa asilimia 99.

Dawa hio imetengezwa kutoka kwa mmea ujulikanao kama Gendarusa ambao wanaume wa kisiwa cha Papua wamekua wakitumia kujizuia kuwashikisha wake zao mimba.

Mmea huo unasemekana kuwa na madini ambayo yanatatiza uwezo wa mbegu za kiume kuzalisha kwa kuzimaliza nguvu na pia kuzifanya kutoweza kuingia katika mayai ya mwanamke.

Profesa Bambang Prajogo, mtafiti mkuu wa mradi huo anasema ana furaha sana kuripoti kwamba dawa hio itaanza kuuzwa mwaka 2016 baada ya miaka mingi ya utafiti na majaribio.

Ingawa dawa hio ya mpango wa uzazi kwa wanaume ina athari zake, kama vile wanaume kuongeza uzazi wanapoitumia wanasayansi wanaamini kuwa athari hizo ni ndogo sana ikilinganishwa na dawa zinazotumiwa na wanawake kwani hauthiri sana homoni zao.

Dawa hio inaweza kumezwa saa moja tu kabla ya tendo la ndoa. Lakini wazee wa jamii hio huchanganya dawa hio na chai na kuinywa dakika thelathini kabla ya tendo la ndoa

Hata hivyo wanaume wanaambiwa wasiwe na wasiwasi kwani wanapata uwezo wa kuzalisha tena siku thelathini baada ya kusitisha utumizi wa dawa yenyewe.