Adebayo apewa likizo binafsi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Emmanuel Adebayo

Emmanuel Adebayor mwenye umri wa miaka 30,mshambuliaji wa klabu ya Tottenham ameruhusiwa kwenda nchini kwao Togo kwa mapumnziko binafsi.

Mshambuliaji huyo atakosa mchezo wa ligi ya Europa dhidi ya Besiktas, kumekua na mashaka juu ya afya yake . Klabu ya Tottenham, haijatoa maelezo zaidi kuhusiana na likizo ya dharula ya mshambuliaji huyo, ambapo katika mtandao wake wa twiita klabu hiyo imesema ilikuwa "Ni jambo binafsi". Adebayor hajaichezea Tottenham toka mwanzoni mwa mwezi Novemba kutokana na maumivu ya nyama za paja na mgongo nakuongeza kuwa pia anamaambukizi mengine ya maradhi

Hata hivyo hali hiyo inadaiwa kuwa huenda itasababisha mchezaji huyo kuchelewa kurejea dimbani.

Image caption Mauricio Pochettino

Mauricio Pochettino anasema nini?

"wachezaji wote walioko kwenye kikosi wako kwenye mipango yangu ya mbele"alieleza kocha huyo raia wa Ajentina. Mchezaji huyo wa zaman wa ameichezea timu yake michezo 12,kwa msimu huu na kufunga magoli mawili.

Meneja Pochettino ameondoa uvumi kuwa nyota huyo anaweza kuondoka kwenye dirisha dogo la usajili la januari.