Mfungwa wa zamani amzomea 'waziri'

Image caption Hicks anadai kuteswa na majasusi wa Marekani kwa ufahamu wa serikali ya Australia

Mfungwa wa zamani wa kambi ya Guantanamo Bay David Hicks amemzomea waziri wa Australia akiituhumu serikali kuwa na habari kuhusu matesi aliyopitia mikononi mwa mwa wanajeshi wa Marekani.

Hicks, aliyeishi miaka mitano na nusu katika kambi hio, alimzomea mkuu wa sheria George Brandis na kusema ni muoga alipokataa kujibu maswali.

Hicks alikifanya kitendo chake wakti bwana Brandis alipokuwa anaongea mbele ya umati wa watu mjini Sydney.

Ripoti iliyotolewa wiki hii na baraza la Senate ililaani shirika la CIA kwa kutumia nuyama na ukatili dhidi ya washukiwa wa kundi la al-Qaeda.

Ripoti hio pia ilionyesha wazi kuwa shirika hilo liliwahadaa wanasiasa na umma kuhusu mpango wake wa mwaka 2001-2007 kuhusu washukiwa wa ugaidi.

Shirika hilo hata hivyo limetetea vitendo vyake baada ya mashambulizi ya 9/11 dhidi ya Marekani likisema kuwa limeweza kuokoa maisha.

Hicks alimzomea Bwana Brandis baada ya hotuba yake katika warsha kuhusu haki za binadamu mjini Sydney mnamo Jumatano.

"jina langu ni David Hicks!" alisema Hicks. "niliteswa kwa miaka mitano na nusu katika gereza la Guantanamo Bay wakati chama chako kikiwa na taarifa kuhusu yaliyokua yananikumba. ''

"muoneni ametoroka, '' alisema Hicks akimtaja waziri kama muoga.

Baadaye Brandis alimtaja Hicks kama gaidi.

Hicks - anayejulikana kama Taliban wa Australia, alikamatwa nchini Afghanistan mwaka 2001 baada ya kushukiwa kwa kulisaidia kundi la Taliban.

Mnamo mwaka 2007, alihamishwa jela hadi nchini Australia baada ya kupatikana na hatia ya kusaidia kuwapelekea silaha magaidi.