Mabibiharusi zaidi ya 100 watoweka China

Haki miliki ya picha Greg Baker AFP
Image caption Wanaume wengi kutoka vijijini China huwa na wakati mgumu kupata wake kutoka maeneo wanakoishi wenyewe

Polisi nchini China wanafanya uchunguzi wa kuwasaka mabibi harusi zaidi ya mia moja wenye asili ya Vietnam ambao walipotea katika kijiji kimoja masikini kaskazini mwa jimbo la Hebei baada ya kuolewa .

Makuwadi waliowauza mabibi harusi kwa wanaume wameshangazwa na kitendo cha kupotea kwa mabibi harusi pamoja na pesa walizozipata makuwadi pia kupotea.

Wanawake hao walikuwadiwa kwa gharama ya dola 16,000 kila mmoja.

Lakini wadadisi wa mambo wanadai kwamba wanaume wa kichina walioko mijini wanapaswa kuwa na fedha za kutosha ili kuwavutia wanawake wa Kichina,na hivyo imewalazimu wanaume wa kichina kununua wanawake kutoka nje ya nchi hiyo kama Vietnam,Cambodia na Burma , zoezi linaloonekana kushika kasi kila uchao wakilenga vijiji hohehahe.