Vita vya Jihadi vyasababisha maafa makubwa

Image caption Hasara inayotokana na mauaji yanayofanywa na makundi ya wapiganaji wa kiisilamu ni vifo vya watu wasio na hatia

Uchunguzi wa BBC umebainisha kwamba mashambulio ya kijihadi yanayofanywa na wapiganaji wa kiisilamu yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 5,000 kote duniani mwezi Novemba.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, mauaji yaliyotekelezwa na kundi la kigaidi la Al Qaeda yanaongezeko kwa ukubwa, kutokana na kuimarika kwa mtandao huo ulioenea katika zaidi ya nchi 14 duniani.

Huku idadi kubwa ya wafuasi wa Al Qaeda wakiwa nchini Iraq, Nigeria, Afghanistan na Syria.

Nchi nne zilizoathirika zaidi kutokana na mauaji yaliyofanywa nawanaopigana jihadi, ni Iraq, Nigeria, Afghanistan na Syria, ikiathirika kwa kiwango kikubvwa zaidi na asilimia 80 ya vifo vyote.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mashambulizi yaliyofanywa na makundi ya jihadi, yaliwalenga waisilamu wa madhehebu ya Shia wale walio wachache pamoja na wasuni wengine

Uchunguzi wa BBC uliofanywa kwa usaidizi wa kituo cha kimataifa cha masomo ya itikadi kali, ulinukuu mashambulizi 664 kufanywa katika mataifa 14.

Uchunguzi huo unalenga kuonyedha idadi ya vifo vinavyotokana na vita vya majihadi kila mwezi na pia kutoa maelezo kuhusu changamoto inayotokana na vita hivyo.

Uchunguzi huo ulionyesha kwamba takriban watu saba walifariki kila saa mwezi Novemba kutokana na vita hivyo, ambavyo vimechochewa na al-Qaeda, na makundi mengine ya wapiganaji wenye kufuata itikadi kama za Al-Qaeda.

Uchunguzi huo ulipokea taarifa ya vifo vya watu 22 kutokana na vita hivyo huku watu 168 wakijeruhiwa vibaya.

Image caption Abu Khattab mwenye umri wa miaka 13 anapata mafunzo kujiunga na kundi la IS

Kundi la wapiganaji la (IS) wanaoendeshea harakati zao nchini Syria na Iraq, walisababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000.

Shambulizi lililofanywa dhidi ya msikiti, mjini Kano, ndilo lilikuwa shambulizi kubwa zaidi kufanywa na wapiganaji wa kiisilamu mwezi Novemba.

Kati ya watu 5,042 waliouawa, wengi wao walikuwa raia wasio na hatia.

Wanajeshi 1,723 ni miongoni mwa waliouawa huku takriban wapiganaji 1,000 pia wakiuawa katika mashambulizi.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Athari kwa maisha ya wananchi wengi wa mataifa yenye vita vya Jihad

Kulingana na uchunguzi huo, Nigeria ndio nchi hatari zaidi kutokana na harakati za Boko Haram wanaolaumiwa kwa mauaji ya watu wengi sana.

Afghanistan ilikuwa nchi ya tatu hatari zaidi kutokana na harakati za wapiganaji waTaliban.

Ripoti hio ilifanywa na shirika la BBC, ICRS na shirika lengine lisilo la kiserikali lenye makao yake mjini London.