Wanaowadhalilisha Watoto kukiona UK

Haki miliki ya picha
Image caption Teknolojia imewaathiri Watoto kuingizwa kwenye vitendo vya ngono

Wataalam wa maswala ya usalama na wataalam wa maswala ya kupambana na uhalifu wanashirikiana kwa pamoja kupambana na picha za mitandaoni zinazowadhalilisha watoto.Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ameeleza.

Cameron amesema vyombo hivi vitawasaka Watu wanaowadhalilisha watoto kingono mitandaoni, vyombo hivyo vitatumia nguvu ileile inayotumika kupambana na magaidi.

Baadae , Waziri Cameron anatarajiwa kutangaza sheria itakayopambana na matumizi mabaya ya mitandao.

Sehemu ya mitandao iitwayo Dark net huwa ya kificho si rahisi kuingiliwa bila kifaa maalum, lakini wataalam wataweza kubaini kiasi cha picha zilizomo zenye kudhalilisha Watoto.

Jitihada zimeelezwa kuanza kuzuia Picha zinazodhalilisha, lakini Cameron anaona kuwa hawatumii matumizi ya kawaida ya Intaneti yanayotumiwa na Watu wote.