Nitaendelea na timu ya McLaren:Jenson

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Jenson Button

Dereva Jenson Button, wa timu ya McLaren, anamatumaini ya kuendelea kuitumikia timu hiyo zaidi.

Jenson Button, amesaini mkataba wa miaka miwili utakaomuweka na timu hiyo mpaka 2016.Button amechaguliwa kuwa timu moja na nyota Fernando Alonso. "kuwa na timu ya Mclaren, kwa Zaidi ya mwaka mmoja ni muhimu ,ila niko hapa kwa ajili kupamba na michuano ya duniaā€¯ Button mwenye miaka 34 awali alionyesha kuchanganyikiwa na ucheleweshwaji wa kutatua mustakabali wake katika timu Mclaren. Mwenyekiti Ron Dennis, ameeleza ilichukua muda kuamua kati ya Button, na mchezaji mwenzake Kevin Magnussen, nani atashirikiana na Alonso, ila ikafikiwa muafaka kwa Button kuchaguliwa. Timu ya McLaren imewatangaza Jenson Button ,Fernando Alonso na Kevin Magnussen kuwa madereva wa timu hiyo kwa msimu ujao wa mwaka 2015.