Mswada wa ugaidi Kenya wawakera wengi

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wakenya wakiandamana kupinga kuzorota kwa usalama nchini Kenya

Bunge la Kenya limepitisha mswada unaolenga kuwapa nguvu zaidi maafisa usalama kukabiliana na ugaidi pamoja na maswla mengine ya usalama.

Wabunge walihusika na mjadala mkali Alhamisi kabla ya mswada huo kupitishwa huku upinzani ukisema kuwa ikiwa itakuwa sheria itakuwa inakiuka haki za wananchi.

Wabunge hao pamoja na mashirika mengine ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa watafanya maandamani ikiwa mswada huo utapitishwa bila ya kufanyiwa mabadiliko ili isikiuke haki za binadamu.

Kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al shabaab limekua likishambulia Kenya mara kwa mara wataalamu wa wakisema kuwa Kenya haina mikakati mizuri ya kudhibiti usalama wake.

Sheria hizo mpya zinampa Rais na mashirika ya ujasusi mamlaka mapya.

Image caption Viongozi wa kiisilamu wamekuwa wakilaumiwa kushindwa kuwazuia waumini wa kiisilamu kujihusisha na vitendo vya kigaidi

Wito ulitolewa kutoka pande zote bungeni kwamba baadhi ya vipengee vya mswada huo ambavyo ni tatanishi kufanyiwa marekebisho.

Badhi ya vipengee hivyo ni:

  • Uhuru wa maafisa wa usalama kuwazuia washukiwa wa ugaidi kwa karibu mwaka mmoja.
  • Uhuru wa mashirika ya kijasusi kudukua simu za watu bila ya idhini ya mahakama.
  • Na mashirika ya habari kupata udhini ya polisi kabla ya kupeperusha au kuchapisha taarifa za uchunguzi kuhusu usalama wa nchi na maswala ya ugaidi nchini.

Mswaada huo sasa utapelekwa kwa kamati ya usalama bungeni kufanyiwa marekebisho kabla ya kupelekwa kwa Rais kuidhinishwa na kuwa sheria.

Wabunge wa upinzani wamelaani mswada huo na kusema unakwenda kinyume na katiba ya nchi.

Image caption Wakenya waliouawa na Al Shabaab mjini Madera wakichimba machimbo ya mawe

Huenda kamati hio ikafanya marekebisho yanayohitajika kwani pande zote zinayaunga mkono.

Rais Kenyatta amesema anataka mswada huo uwe sheria haraka iwezekanvyo.

Vipengee vingine vye sheria hio inayopendekezwa vinampa Rais mamlaka ya kuwafuta kazi na kuwaajiri maafisa wakuu wa usalama, kuyapa mashirika ya ujasusi uhuru wa kuwakamata washukiwa wa ugandi na sharti kwamba watu wanaopatikana na silaha katika sehemu za maombi kufungwa jela miaka 20.