Yaya apatikana na hatia Uganda

Haki miliki ya picha no credit
Image caption Yaya Jolly Tumuhirwe anasema alimchapa mtoto kwa sababy naye alikuwa anapwa na mamake mtoto huyo

Yaya wa Uganda ambaye alinaswa kwa kanda ya video akimchapa na kumkanyaga mtoto mdogo amepatikana na hatia ya ukatili.

Atafikishwa mahakamani tarehe 15 Jumatatu Disemba kupokea hukumu .

Jolly Tumuhirwe aliambia mahakama kuwa alilazimika kufanya kitendo chake kwa sababu mamake mtoto huyo aliwahi kumchapa mara kadhaa.

Alipokuwa anaondoka kortini mamake mtoto Angella Mbabazi, alikanausha madai ya Jolly akisema hajawahi kumgusa Jolly hata wakati mmoja.

Alihoji madai ya Jolly akisema angewezaje kumchapa msichana huyo wa kazi na kisha amuache na mtoto wake?

Awali tuhuma dhidi ya Jolly kuwa alimtesa mtoto huyo, yalitupiliwa mbali na mwendesha wa mashitaka wakisema ingekuwa vigumu ,kuweza kuyathibitisha

Huenda akafungwa jela miaka 5 jela kwa kumchapa na kumjeruhi mtoto.