Watu 3 wauawa katika vita Somalia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanajeshi wa serikali ya Somali .Vita vimezuka katika ya wanajeshi wa somali na wanamgambo wa Alhu Sunna

Mapigano kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo katikati ya Somali yamesababisha vifo vya watu watatu.

Pande hizo mbili zinapigania udhibiti wa jimbo la Galgadud ambalo linatarajiwa kuwa miongoni mwa majimbo ya serikali ya Somali.

Pande zote zinadai kudhibiti mji mkuu wa jimbo hilo Dusa Mareb na kuna mapigano mengine kusini magharibi kutoka kwa kundi la Ahlu Sunna,ambalo ndio kundi la kwanza lililowafukuza wapiganaji wa Alshabaab katika eneo hilo mwaka 2011 wakisaidiwa na wanajeshi wa Ethiopia.

Kundi la Ahlu Sunna limekuwa likiunga mkono Serikali ya Mogadishu lakini sasa viongozi wake wanasema kuwa wametengwa katika mpangilio mpya wa utawala.