Zaidi ya abiria 100 wazama DRC

Ziwa Tanganyika upande wa Tanzania Haki miliki ya picha other

Ripoti kutoka Jamhuri ya Demokrasi ya Congo zinaeleza kuwa watu zaidi ya 100 wanafikiriwa kuwa wamekufa katika ajali ya feri.

Jahazi iliyojaa abiria imezama katika Ziwa Tanganyika kusini-mashariki mwa nchi siku ya Alkhamisi.

Waziri wa usafiri wa jimbo hilo la Katanga, Laurent Sumba Kahozi), aliliambia shirika la habari la Ufaransa kuwa miili kama 129 imepatikana.

Inaarifiwa watu 232 walinusurika.

Ajali hiyo ilitokea Alhamisi usiku kaskazini mwa jimbo la Katanga baina ya miji ya Moba na Kalemie.

Waandishi wa habari wanasema ajali kama hizo zinatokea kawaida kwa sababu feri mara nyingi zinakuwa zimejaa mno.