Dunia yaambiwa isiisahau Sudan Kusini

Mapambano Sudan Kusini Haki miliki ya picha AP

Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu, ICRC, limeonya kuwa mwaka mmoja baada ya ghasia kuzuka Sudan Kusini mapambano bado yanaendelea baina ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji na kuhatarisha raia.

Mkuu wa ICRC nchini humo, Franz Rauchenstein, alisema ingawa waandishi wa habari wameipa mgongo Sudan Kusini, wale walionasa katika vita hivyo haifai kuwasahau.

Mapigano yalizuka Disemba mwaka jana baina ya wanajeshi wa Rais Salva Kiir na wale watiifu kwa makamo wake wa rais wa zamani, Riek Machar.

Watu kama milioni moja na nusu wamepoteza makaazi na mashirika ya misaada yanasema msaada wa kimataifa unahitajika kuepusha upungufu mkubwa wa chakula.