Jenerali David Ssejusa arejea Uganda

Image caption Aliyekuwa mkuu wa vikosi vya ujasusi nchini Uganda Jenerali David Ssejjusa aliyeishi uhamishoni nchini Uingereza tangu Aprili,2013

Aliyekua mkuu wa vikosi vyote vya ujasusi nchini Uganda Jenerali David Sejjusa amerejea nyumbani kutoka uhamishoni Uingereza bila kutarajiwa. Jenerali Sejusa alitoroka nchini Uganda mwaka jana baada ya kumshutumu Rais Museveni kuwa alikuwa akimuandaa mwanaye kuchukua uongozi wa nchi baada ya kustaafu kwake.

Kurejea kwake kwa siri bila kukamatwa kuna leta maswali mengi kwa wananchi nchini Uganda.

Image caption Rais Yoweri Museveni wa Uganda

Jenerali Ssejusa aliwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe, jana alfajiri akitokea Uingereza alikokuwa takriban miaka miwili iliyopita, tangu mwezi Aprili 2013. Katika uwanja wa ndege alipokelewa na mkuu wa kikosi cha ujasusi cha Uganda Roney Baria, dada yake na mwanasheria wake Ladslaus Rwakafuzi, ambaye amesema Jenerali Ssejussa amerudi nyumbani kwa sababu ni haki yake kama raia wa Uganda kwa mujibu wa katiba. Kurejea kwake kumewashangaza raia wengi wa Uganda kwani mpaka sasa hajakamatwa ikizingatiwa kuwa mwaka jana aliandika barua kwenye gazeti moja nchini Uganda akikashfu utawala wa Rais Yoweri Museveni kuwa alikuwa akimwaandaa mtoto wake wa kiume Brigedia Muhozi Kaneirugaba kuwa mrithi wake mara atakapoachia ngazi. Shutuma ambazo Rais Museveni amekuwa akizipinga.

Msemaji wa serikali ya Uganda Ofono Opondo ameiambia BBC kuwa Jenerali Ssejusa aliwasili na serikali ya Uganda akiomba kurudi nyumbani, na serikali ikakubaliana na ombi lake na

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Askari wa jeshi la Uganda wakitoa heshima wakati wa mafunzo

na kugharamia usafiri wake kutoka Uingereza.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliozungumza na BBC wamesema litakuwa jambo la kuipongeza serikali ya Rais Museveni kama haita kugharamia usafiri wake kutoka Uingereza.mchukulia hatua Bwana Ssejusa, na hilo jambo litaonyesha ukomavu wa kisiasa kwa serikali kuvumilia uhuru wa wananchi wake wa kutoa mawazo. Wengine wamempongeza Jenerali Ssejusa kwa kuamua kurejea nyumbani, wakiwataka watu wengine wanaoishi uhamishoni kwa sababu za kisiasa kuiga mfano wa Bwana Ssejusa.