Nchi zenye Ebola kufutiwa madeni

Haki miliki ya picha NIH SPL
Image caption Miradi ya kutafuta chanjo ya Ebola bado inaendelea katika juhudi za kupambana na maradhi hayo hatari

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imetaka mataifa na mashirika yanayotoa mikopo kutafakari kwa kina uwezekano wa kufutilia mbali mikopo iliyopewa mataifa yaliyoathirika zaidi na Ebola.

Ripoti hiyo Tumeya Uchumi ya Africa UNECA, pia inasema iwapo Ebola itathibitiwa katika mataifa Sierra Leone, Guinea na Liberia, athari zake kwa uchumi zitakuwa ndogo sana katika mataifa mengine barani.

UNECA inasema athari za Ebola kwa uchumi wa Sierra Leone, Guinea na Liberia, ni kubwa mno kuhitaji kufutiliwa mbali kwa madeni. Hii itaruhusu nchi hizo tatu kuanza upya na kujiinua pale ugonjwa huo utakapokabiliwa.

Ripoti hiyo imesema kuwa biashara nyingi zinaendelea kufungwa kila wiki na wafanyikazi kupoteza ajira zao, huku sekta kama vile Utalii, ujenzi na elimu zikiathirika pakubwa. Lakini nje ya mataifa haya matatu, athari itakuwa ndogo sana barani Afrika.

Hii ni kwa sababu uchumi wa nchi hizo ni chini ya asilimia moja barani Afrika. Aidha ripoti hiyo imeonya kuwa sekta ya afya katika mataifa hayo matatu huenda ikaathirika zaidi na kusababisha ongezeko la magonjwa mengine kama vile Malaria, na homa ya majano.

Mfumuko wa bei ya vyakula pia umeshuhudiwa katika nchi hizo.

Mbali na haya, mayatima wameongezeka sana huku wakiwa hawana wa kuwatunza.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa jijini Addis Ababa, hii lewo sasa imetaka jamii ya kimataifa kuimarisha usaidizi unaotolewa kwa mataifa yaliyoathirika, na hasaa katika kutoa fedha zailizoahidiwa kukabiliana na Ebola.

Pia mataifa hayo yametakiwa kuhakikisha kuwa wanaougua, wanapata matibabu ya haraka ili kuzuia ugonjwa huo kusambaa hata zaidi.