Askofu mwanamke achaguliwa Uingereza

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mchungaji Libby lane amechaguliwa mwanamke wa kwanza kuwa askofu nchini Uingereza

Kanisa la Uingereza limemchagua askofu wa kwanza mwanamke.

Mchungaji Libby Lane atakuwa askofu wa Stockport mnamo mwezi January ,na kumaliza ukiritimba wa wanaume kuwa maaskofu katika kanisa hilo.

Amesema kuwa amefurahishwa na hatua hiyo.

Kanisa la Uingereza liliwachagua wanawake mara ya kwanza kama makuhani mnamo mwaka 1994.

Wanawake tayari wameruhusiwa kuwa maaskofu katika maeneo mengine ya jamii ya kianglikana ,ikiwemo Marekani na kusini mwa Afrika.