Marufuku manunuzi Jumapili,Hungary

Haki miliki ya picha c
Image caption Waandamanaji nchini Hungary

Bunge nchini Hungary limepiga kura ya kupendekeza kusitisha kufanya manunuzi ya vitu katika maduka makubwa siku ya jumapili kuanzia mwezi March mwakani.

Hatua ya pendekezo hilo la bunge imekuja kutokana na nchi hiyo kutohitaji vurugu za aina yoyote siku ya jumapili na kuwataka wanafamilia kutulia nyumbani.

Baadhi ya raia wamepinga hatua hiyo ya serikali kwa kufanya maandamano wakitetea mtazamo wao wa masoko hayo kuendelea hadi siku ya jumapili.

Waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban amepigwa vikali kutokana na pendekezo hilo na kudai kuwa ni mapendekezo yanayotokana na mazingira ya rushwa.

Raia mmoja kati ya watano nchini humo hufanya manunuzi siku ya jumapili hali ambayo wanasema upigaji marufuku huo utawasababishia usumbufu mkubwa.

Nayo taasisi ya wamiliki wa maduka imeonya kuwa hatua hiyo ya serikali inaweza kusababisha kupotea kwa ajira zaidi ya 20,000.