Boko Haram tishio kwa Wanajeshi Nigeria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Operesheni dhidi ya Wanamgambo wa Boko Haram imekuwa haizai matunda nchini Nigeria

Wanajeshi 54 wamehukumiwa adhabu ya kifo na mahakama ya Kijeshi nchini Nigeria kwa kukataa kupambana na Wanamgambo wa kiislamu, Boko Haram.

Wanajeshi walikutwa na hatia ya uasi ,kushambulia na uoga.Wanajeshi hao wanashutumiwa kukataa kupigana kurudisha miji mitatu iliyokuwa ikishikiliwa na Boko Haram mwezi Agosti.

Mwanasheria wa Wanajeshi hao amesema wamehukumiwa kifo cha kupigwa risasi na kikosi maalum huku Wanajeshi wengine watano wakiachiliwa.

Vikosi vya kijeshi vya Nigeria vimedai kuzidiwa silaha na Boko Haram, kwa kuwa hawapatiwi silaha za kutosha kupambana na Wanamgambo.

Boko Haram wanapambana kuunda himaya ya kiislamu kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.