Mwalimu apigwa makofi na mtawa

Image caption Watawa nchini Thailand

Mwalimu mmoja wa somo la kiingereza amepigwa makofi na mtawa baada ya kutoa kiti chake katika treni kwa wanawake wawili.

Jamaa huyo anayejulikana kama jeff katika mtandao wa facebook alikuwa katika treni iliokuwa ikisafiri kutoka Bankok kuelekea Phitsanulok nchini Thailand wakati alipojaribu kutatua hali yenye utata kwa kutoa kiti chake kwa wanawake wawili ili kuweza kukaa na mtawa huyo.

Lakini kulingana na mtumiaji mmoja wa mtandao wa facebook ambaye aliweka video hiyo katika mtandao,Mtawa huyo hakufurahishwa na mawanamume huyo kukaa chini na vilevile neno fine ambalo alielewa kuwa Kwai linalomaanisha Bufallo kwa lugha ya Thai.

Baada ya kumzaba makofi mara tatu ,mtawa huyo aliondolewa katika treni hiyo na maafisa wa polisi .

Jeff baadaye alisema kuwa alitaka kukisahau kisa hicho katika taarifa iliowekwa katika mtandao na jirani yake Noojeab Kuntao.