Alastair Cook kuvuliwa unahodha

Haki miliki ya picha PA
Image caption Nasser Hussain

Nahodha wa zamani wa timu ya kriketi ya Uingereza Nasser Hussain amesema bado kuna muda wa kuweza kumbadili nahodha wa sasa wa timu hiyo Alastair Cook kabla ya kombe la dunia.

Nasser Hussain amesema"uingereza inapaswa kubadili nahodha hana msaada kwa timu Alastair ameshindwa kufunga timu ya Uingereza katika michezo ya siku hivi karibuni.

Kocha mkuu Peter Moores amesema hakuna uhakika kama Cook ataendelea kuwa nahodha kwa mpaka kwenye kinyanganyiro cha kombe la dunia la kriketi.

Huku mkurugenzi mtendaji wa bodi ya kriketi Paul Downton ameshangazwa kama nahodha huyo hato ongoza timu hjiyo kwenye michezo ya kombe la dunia.

Desembe 21 kocha Peter Moores atatangaza kikosi chawachezaji 16 watakao cheza michezo dhidi ya Australia na India.

Uingereza hawaijawahi kutwaa ubigwa wa dunia wa kriketi na wameshindwa kuvuka robo fainali toka mwaka 1996.