M'marekani ahusishwa na fedha bandia UG

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Fedha bandia.Raia mmoja wa marekani amehusishwa na utengenezaji fedha bandia nchini Uganda.

Mamlaka ya Marekani imemkamata raia mmoja wa taifa hilo kwa kuongoza kashfa ya kimataifa ya fedha bandia,BBC imebaini.

Ryan Gustafson mwenye umri wa miaka 27 alishtakiwa kwa njama ya kuwa na fedha bandia nje ya Marekani baada ya fedha hizo kutumika katika biashara tofauti za Marekani.

Shirika la kijasusi la Marekani lilifuatilia fedha hizo hadi Kampala ,ambapo walibaini kuna njama ya fedha hizo bandia inayotengeza yuro,rupee pamoja na fedha tofauti za nchi za Afrika.

Mshukiwa huyo anakabiliwa na kifungo cha miaka 25 gerezani.

Haki miliki ya picha Policia Italiana
Image caption Fedha bandia

Maajenti wa FBI waligundua fedha hizo zinatumwa kutoka Uganda.

Alama ya kidole kutoka kwa kifurushi cha fedha hizo ilitoa maelezo ya fedha hizo kutoka kwa bwana Gustafson,raia wa Marekani.

Shirika hilo la maafisa wa ujasusi lilishirikiana na mamlaka ya Uganda ili kuanzisha uchunguzi wa siri kwa lengo la kununua fedha hizo kutoka kwa mshukiwa huyo.

Alikamatwa ,na msako kufanywa katika nyumba yake ambapo fedha bandia za Uganda,Francs za Congo,Cedis za Ghana,Rupees za India na Yuros pamoja na vifaa vya kutengeza fedha bandia.

Mamlaka ya Marekani inakisia kwamba washukiwa hao waliingiza takriban dola millioni 2 fedha bandia katika soko.