Sony yasitisha utoaji Sinema

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kim Jong-un

Kampuni ya Sony imetangaza kusitisha mpango wake wa awali wa kutaka kutoa na kuzisambaza sinema za kuigiza nchini Marekani zinazomhusu kiongozi wa Korea kaskazin Kim Jong-un

Wiki iliyopita kampuni ya Sony ilitangaza dhamiri yake hiyo, lakini ikakumbwa na upinzani wa makampuni mengi ya sinema kukataa kusambaza video hizo.

Awali wadukuzi wa kimitandao walionya watu wasiende kuangalia sinema hizo zinazojulikana kwa jina la Interview.

Kampuni inayotengeneza sinema hizo ilisema kuwa mpango wake umeathiriwa na udukuzi uliofanywa kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Wachunguzi wa kimitandao nchini Marekani wanaamini kuwa Korea Kaskazini ni kweli ilikuwa ikifuatilia nyendo za kimitandao za kampuni ya Sony ambapo picha hizo za video ya Interview zilisambazwa hata kabla ya Sony wenyewe kufanya hivyo.