Flora Mabasha adai talaka

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Flora Mbasha

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili nchini Tanzania,Flora Mbasha,amekwenda katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar-Es-Salaam,akiomba kuvunjwa kwa ndoa yake na mumewe Emanuel Mbasha.

Flora amefungua kesi ya madai namba 64 ya mwaka huu kesi ambayo inasikilizwa na hakimu mkazi,Devota Kisoka.

Flora anadai kuomba kuvunja ndoa hiyo na apewe talaka ni kutokana na tabia ya mumewe kumpiga,kumnyanyasa na kushindwa kumpatia matibabu.

Katika hati hiyo ya madaianaendelea kudai kwamba mgogoro wao waliwahi kuufikisha kwa ustawi wa jamii,kwa ajili ya upatanishi lakini ilishindikana wakashauriwa walifikishe suala lao mahakamani.

Flora anaiomba mahakama itoe talaka,iamuru aendelee kukaa na mtoto,matunzo ya mtoto yatoke kwa mbasha na wagawane mali walizochuma pamoja.