Alala barabarani kuchangisha fedha

Image caption Dominique Harrison Bentzen mwanafunzi aliyeamua kulala katika barabara ili kuchangisha fedha za mwanamume aliyemuokoa kupata nyumba.

Mwanafunzi anayesoma katika chuo kikuu cha Lancashire nchini Uingereza amekuwa akilala katika barabara za mji wa Preston ili kuchangisha fedha za kumsaidia mwanamume mmoja asiye na makao ambaye alimuokoa.

Mtu huyo anayejulikana kama Robbie alimpatia Dominique Harrison Bentzen pauni zake 3 alizokuwa nazo ili kupanda taxi baada ya mwanafunzi huyo kupoteza kadi zake za banki alipotoka usiku mwezi Disemba.

Msichana huyo alikataa, lakini akasema ameguswa sana na mtu huyo hatua iliomfanya kuanza kuchangisha fedha ili kumsadia kupata nyumba.Ijapokuwa lengo lake lilikuwa kuchangisha pauni 500,amefanikiwa kuchangisha pauni 20,000 kufikia sasa.

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Central Lancashire waliwataka raia kutoa pauni 3 kila mmoja wao na kusema kuwa ameshangazwa na watu waliochangisha kitita hicho cha fedha.

Sikupanga kupata fedha hizi kwa hivyo kwa sasa natafuta ushauri ,aliiambia BBC,lakini umuhimu ni ni kutumia pauni 1,500 kumsaidia Robbie.