Raia wa Australia afungwa kwa mauaji

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mto wa kuchegama ndio ulitumika kuondoa uhai wa watoto wadogo ndugu wawili.

Raia wa Australia aliyezaliwa Tanzania na ambaye sasa anaishiye Melbourne,Australia,Charles Mihayo mwenye umri wa miaka 36,aliyekuwa akituhumiwa kwa mauaji ya binti zake wawili,amehukumiwa kifungo cha maisha jela.

Mihayo ametiwa hatiani baada ya mahakama kujiridhisha kwa ushahidi uliothibitisha kwamba aliwaua binti zake, Indiana aliyekuwa na umri wa miaka mitatu na Savannah aliyekuwa na umri wa miaka minne kwa kuwaua kwa kuwabana kwa mito ya kulalia na hivyo kukosa hewa.

Waendesha mashtaka walisema kwamba, Mihayo alitenda kosa hilo baada ya kuingia kwenye mgogoro mzito na mama wa watoto aliyewahi kuwa mkewe kwa minajili ya kujilipiza kisasi.

Akitoa hukumu hiyo jaji wa mahakama kuu ya Victorian,Lex Lasry alisema ugomvi na mkewe haikuwa sababu ya kujiaminisha kutenda kosa la mauaji na kushangazwa na namna mtuhumiwa alivyotumia nafasi ya ugomvi na mkewe wa zamani kuwaua watoto ili kupunguza machungu yake.

Inaelezwa kuwa Mihayo alituma ujumbe mfupi wa maneno kwa mtalaka wake kumfahamisha kuwa ameshinda na anakubali kupoteza haki yake ya kuwaona watoto hao, kisha akawapiga picha watoto hao wakicheza muziki muda mfupi kabla na kuwaweka pamoja na kuwabana pumzi kwa kutumia mito ya kulalia.

Kisha alipiga simu kwa polisi na walipowasili eneo la tukio, aliwaambia "nimekamilisha,nimewaua watoto.