Masharti kwa wimbo wa taifa China

Haki miliki ya picha BBC CHINESE
Image caption Bendera ya China

Wimbo wa taifa wa China hautaruhusiwa kuchezwa tena maharusini , matangani, au kwenye hafla zozote zisizo za kiserikali.

Serikali imesema kuwa wimbo wa taifa utaruhusiwa tu kuchezwa katika baadhi ya hafla za kiheshima na zenye maafisa wakuu wa serikali.

Amri hii imetolewa ili kuhakikisha heshima kwa wimbo wa taifa ambao ni ishara ya uhuru wa taifa pamoja na uzalendo, ustawi , nchi yenye nguvu na watu wenye utaifa. Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika la habari la serikali, Xinhua.

Wimbo huo unaojulikana kama "The March of the Volunteers" unaweza kuchezwa katika sherehe muhimu za serikali au mikutano ya kisiasa , hafla za kidipllomasia au hafla zenye wageni wakuu wa kimataifa.

Wimbo huo pia unaweza kuchezwa wakati wanariadha wa China wakiwa wanavishwa medali zao walizoshinda katika mashindano ya kimataifa.

Watakaovunja sheria hio watakosolewa na kisha kuadhibiwa.

Wimbo huo ulitungwa mwaka 1949 na unajumuisha mistari ya kuwaasa wanjeshi kutoogopa vita licha ya kukabiliwa na maadui.