Msako kwenye mtandao wa Instagram

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Justin Bieber anasema amepoteza wafuasi zaidi ya milioni moja.

Mtandao wa kijamii wa Instagram umefuta mamilioni ya akaunti za watumiaji wa mtandao huo katika msako wake wa kufuta akaunti bandia zilizokuwa zikituma ujumbe ovyo ovyo kwa watumiaji wengine wa mtandao huo.

Watu waliokuwa wanatumia mtandao huo na kuwa na wafuasi wengi, walilalamika sana kufuatia hatua hio na kuitaja kama "Instagram Rapture".

Kama Facebook, Instagram hufuta akaunti kadha ili kuzuia ujumbe unaotumwa na akanuti wa watu wasiojulikana au akaunti bandia kwa mtumiaji na pia kuzuia watumiaji wa mtandao huo kununua 'likes', ili kuonekana kuwa maarufu.

Mwanamuziki Akon anasemekana kupoteza asilimia 56 ya wafuasi wake katika msako huo wa akaunti bandia.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Justin Bieber

Wanamuziki wengine wakiwemo, Justin Bieber alipoteza wafuasi milioni 3.5 na kampuni pia hazikusazwa kwani kampuni ya Wellington Campos, nayo ilipoteza wafuasi milioni 3.2.

Mtandao wa Instagram ulikuwa tayari umetoa onyo kwa watumiaji wake kwamba baadhi ya akaunti za watumiaji wake zitakuja kufutwa.

"tumekuwa tukiona akaunti bandia kwenye Instagram na ilibidi tuzifute maana zinatuma ujumbe kwa akaunti za watumiaji wa kweli wa mtandao huo, '' alisema mkuu wa kampuni hio,Kevin Systrom.

"kama sehemu ya jitihada zetu, tutafuta akaunti hizo na hazitawahi tena kuwa na wafuasi. Ina maana kwamba baadhi yenu, mtaona mabadiliko katika akaunti zenu,'' alisema Bwana Systrom.

Katikakujibu hatua hio ya Instagaram, watumiaji wengi walitoa matamshi makali hasa waliofutiwa akaunti zao.

Mwanamzuki Mase, aliyepoteza wafuasi wake milioni moja alifuta akaunti yakebaada ya kudaiwa kulipa ili apate wafuasi.