Mwanamume auwa ili kujiliwaza Brazil

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Tiago Gomes Da Rocha anayedaiwa kuwaua watu 39 brazil.Muuaji mwengine anayedaiwa kuwaua watu 41 amekamatwa nchini humo na kukiri kwamba yeye hufanya hivyo ili kujiliwaza.

Mwanamume mmoja raia wa Brazil ambaye amekiri kuwa muuaji wa zaidi ya watu 40 amesema kuwa yeye hufanya hivyo ili kujiliwaza.

Sailson Jose Das Gracas amewaambia maafisa wa polisi kwamba huwatafuta wanawake weupe na kuwachunguza kwa mwezi mmoja kabla ya kuwaua.

Muuaji huyo amekiri kuwaua wanaume 41 wanawake na watoto baada ya kukamatwa kwa kumdunga kisu mwanamke mmoja hadi kumuua.

katika mauaji ya miaka tisa ambayo hayakuripotiwa ,Graca anadai kuwaua wanawake 37,wanaume wawili na mtoto mmoja wa miaka miwili katika eneo la Rio de Jeneiro linalojulkana kama Baixada Fluminense.

Amewaambia maafisa wa Polisi, ''mimi huwachunguza waathiriwa ,kungoja kwa kipindi cha mwezi mmoja ama hata juma moja ikitegemea eneo lenyewe,hujaribu kujua mahala anapoishi,vile familia yake ilivyo na iwapo angepita barabarani ,ningemwangalia kuchunguza nyumba anayoishi.

Aliendelea''Na ifikiapo alfajiri mimi hutafuta mwanya wa kuingia katika nyumba yake na kumuua'',.

Afisa mkuu wa polisi Pedro Henrique Medina kutoka kituo cha polisi cha Baixada amesema kuwa Gracas alikiri mwenyewe kuhusu mauaji hayo baada ya kushikwa akimuua mmoja ya waathiriwa.

Amesema kuwa anaamini ushahidi wake kwa kuwa ni muuaji pekee anayeweza kuelezea kilichojiri.

Graca anasema kuwa yeye hujisikia mtulivu anapotekeleza mauaji .

''Iwapo sijafanya kitendo hicho mimi hujisikia kubabaiki na kuwa na wasiwasi mwingi katika nyumba yangu''.