Nigeria:Mgomo wasitishwa viwandani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption India hununua kiwango kikubwa cha mafuta kutoka nchini Nigeria

Wafanyakazi katika sekta ya mafuta nchini Nigeria wamesitisha mgomo ulioanza mapema juma hili ambapo walikuwa wanalalamikia hali mbovu katika viwanda vya usafishaji mafuta na pia ubovu wa miundombinu.

Vyama viwili vikuu nchini, Pengassan na Nupeng, vilisema kuwa Serikali iko tayari kuchukua hatua kuhusiana na malalamiko yao.

Uchumi wa Nigeria, unaotegemea pakubwa mauzo ya mafuta katika mataifa ya kigeni, umevurugika pakubwa na kuporomoka kwa bei ya mafuta duniani.

Benki Kuu imetangaza hatua mpya za kuthibiti sarafu katika hatua ya kulinda sarafu ya Nigeria ya Naira. Juma hili Naira ilifikia kiwango cha chini sana ikilinganishwa na Dolari ya Marekani.