Bondia Amir Khan kuelekea Pakistan

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kushoto ni Amir Khan

Bondia wa uingereza Amir Khan atakwenda Pakistan, mwisho wa mwezi kuonyesha ushirikano kwa waathirika wa mauaji ya shule Peshawar.

Katika tukio la mauaji hayo watu 141 waliuwa na wanamgambo wa Taliban.

Wazazi wa bondia huyu walizaliwa nchi Pakistan,Khan atatoa msaada wa mchango kwa ajili ya ujenzi mpya wa shule.

"Nitakwenda Pakistan siku chache zijayo nataka kusema ukweli na kuwambia kinachotokea ni makosa, nataka iwe nchi bora"

Khan mwenye miaka 28 anatarajia kusafiri kwenda Pakistan kati ya krisimas na mwaka mpya.