Elton John na David kufanya harusi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Elton John na mpenziwe david furnish

Msanii Sir Elton John atafanya ndao yake na mwana filamu David Furnish baadaye jumapili.

Kulingana na gazeti la the Independent nchini Uingereza, Elton John mwenye umri wa miaka 67 atafunga ndoa na mpenziwe wa miaka 20 katika nyumba yao ya Windsor ,na wote wawili wataweka picha ya harusi yao kwa instagram.

Wapenzi hao wa jinsia moja ndio wa kwanza kuunganishwa mwaka 2005 lakini wanataka kuimarisha uhusiano wao zaidi miaka tisa baadaye, baada ya sheria za ndoa za jinsia moja kuhalalishwa nchini Uingereza.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Msanii Elton john

''Tulikuwa na sherehe kubwa tulipounganishwa kiraia lakini tutafanya harusi,''Elton John alikiambia chombo cha habari cha Sky News mapema mwaka huu.

''Nadhani ni vizuri kuchukua fursa ya sheria hizi mpya ili kusheherekea.Tuna bahati sana katika taifa hili kuweza kupata fursa kama hii''.