Ronaldo azindua sanamu yake

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Cristiano Ronaldo

Cristiano Ronaldo amezindua sanamu yake ya kumuenzi kwa mafanikio yake, katika mji aliozaliwa wa Funchal kwenye Kisiwa Madeira.

Akizungumza katika uzinduzi huo maalumu huku akizungukwa na Familia yake pamoja na Maelfu ya Mashabiki, Ronaldo alieleza “Huu ni wakati maalumu kwangu, kuweka Sanamu yangu!”

Dolores Aveiro mama yake Ronaldo aliongeza kwa kusema"Ronaldo hajawahi kusahau asili yake”

Sanamu hiyo yenye Urefu wa Mita 3.4 ni sehemu ya mkusanyiko wa Mataji na Tuzo mbalimbali ambazo amezitwaa katika maisha yake ya Soka na kuhifadhiwa kwenye Makumbusho yake maalum hapo Kisiwani Madeira zikiwemo tuzo za Ballon d'Or.

Ronaldo amefunga jumla ya magoli 34 katika michezo 27 msimu huu, na anawania tuzo ya mchezaji bora wa dunia.