Baraza la Michezo Tanzania lafanya uchaguzi

Image caption Bendera ya Tanzania

Waziri wa habari Vijana Utamaduni na Michezo Dr. Fennella Mukangara ameteua baraza jipya la michezo Tanzania (BMT) ambalo litakuwa likisimamia shughuli zote za kimichezo.

Mukangara amemteua Dioniz Malinzi kuwa mwenyekiti wa baraza la michezo la Taifa, kwa upande wa wajumbe amewateua tena Jamal Rwambow,Alex Mgongolwa ,Jeniifer mmasi Shanga na Zainab Mbiro .

Wajumbe wapya Zacharia Hans Pope,Mohamad Bawaziri,Zainab Vullu mbunge wa viti maalum,Adam Mayingu mkurugenzi wa PSPF ,Cresscntius Magori na John Ndumbaro.