Mwaka 2015 Utakua mgumu kwa Ferrari

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ferrari

Mwenyekiti wa timu ya magari ya Ferrari Sergio Marchionne anahisi msimu wa mwaka 2015 utakua mgumu.

Sergio Marchionne anapatwa na wasiwasi huku timu ya Ferrari ikiwa imemtimua mkuu wa timu Marco Mattiacci, na kumkabidhi majukumu Maurizio Arrivabene, kuwa kiongozi mpya.

Pia kuna kuna mabadiliko kwa upande wa madereva ambapo Sebastian Vettel, ndie atakua dereva kinara baada ya Fernando Alonso ,kutimkia timu ya McLaren.

Hata hivyo Marchionne anaamini ujasiri unaweza kuwaokoa kupambana na wapinzani wao haswa timu ya Mercedes.

Timu ya Ferrari haikufanya vizuri katika msimu wa mwaka 2014.