Kitisho cha Usalama: Polisi auawa, Kenya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi nchini Kenya katika doria

Askari mmoja ameuawa na mwingine akiwa mahututi baada ya kushambuliwa kwa kupigwa risasi kaskazini mwa Kenya.

Askari hao wa Kenya wanadaiwa kushambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa kundi la Al Shabaab.

Askari hao wa jeshi la polisi kikosi cha ziada walikutwa na kisa hicho mjini Wajir kaskazini mwa Kenya usiku wa kuamkia leo.