Polisi mzungu kutoshtakiwa Marekani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Marekani Barack Obama

Polisi mzungu anayetuhumiwa kwa kumpigia risasi Mmarekani mweusi, April mwaka huu hatokabiliwa na mashtaka yoyote.

Mwendesha mashtaka katika mji wa Milwaukee nchini Marekani Amesema askari huyo Christopher Manney, alichukua hatua hiyo kwa lengo la kujihami baada ya kukabiliwa na Dontre Hamilton katika moja wapo ya bustani iliyopo mjini humo.

Askari huyo alimpiga risasi Hamilton, ambaye aliyekuwa na historia ya matatizo ya akili, baada ya kumng'ata shingoni.

Kifo cha Dontre Hamilton bado hakijaibua hisia za wengi ikilinganishwa na kifo cha Michael Brown na Eric Garner ambavyo vimesababisha kufanyika kwa maandamano ya nchi nzima yenye lengo la kulaani ukatili huo.

Familia ya Hamilton imekasirishwa na kauli ya mwendesha mashtaka huyo hivyo imeomba uchunguzi zaidi ufanywe na serikali kuu.