Kwa wivu,Mume amjeruhi mkewe kwa shoka

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Muonekano wa Malaysia

Mama mwenye watoto watatu anapata matibabu hospitalini nchini Malaysia baada ya mumewe kuvamia mikono yake na miguu nakumcharanga kwa shoka la kucharangia nyama,na baadaye mwanamume huyo kujinyonga .

Mama huyo anatajwa kama K Menaga,amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Kluang upande wa kusini mwa jimbo la Johor baada ya shambulio hilo hatari lililotokea mapema mwezi huu.

Ingawa taarifa kutoka hospitalini hapo zinaarifu kuwa mama huyo ameshatolewa katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya hali yake kuendelea vyema,na amelazwa katika wodi ya wagonjwa wa kawaida.

Inasemekana mume wa mwanamke huyo ana umri wa miaka 47 na asiye na kazi maalumu baada ya kumcharanga mkewe na kuona damu tele imtokayo mkewe, aliamua kunywa sumu na baadaye kujinyonga .Mke wa bwana huyo alikuwa akifanya kazi ya kuosha vyombo huko Singapore kwa muda wa miaka 15 sasa .

Majirani wanaeleza kuwa familia ya mwanamke huyo ilikuwa inaishi kwa kutegemea mshahara wa mwanamke huyo, wakati mumewe alikuwa hana chanzo cha mapato.Na mwanamke huyo alikuwa na utaratibu wa kurejea nyumbani kwake mara moja kwa mwezi kuwaona watoto wake akiwemo mama mkwe wake.

Mashuhuda hao wanasema kwamba,kila mwanamke huyo arejeapo kutoka kibaruani, mumewe alikuwa akimshutumu kwa kukosa uaminifu na kumshutumu kuwa ana bwana ambaye humrejesha kutoka Singapore,nao polisi wameeleza kuwa matokeo ya tukio hilo ni wivu wa mwanamume huyo,na baada ya tukio hilo kaka wa mwanamke huyo anaeleza kuwa watoto wa mwanamke huyo wamechukuliwa na jamaa zao kwa matunzo.