Ebola bado tishio

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Peter Piot

Shirika la Afya Duniani limesema ugonjwa wa Ebola hautaweza kudhibitiwa kikamilifu katika kipindi cha mwaka mmoja unaokuja.

Mwenyekiti kutoka kitengo maalumu kinachoshughulikia ugonjwa huo, kutoka katika Shirika la Afya Duniani Profesa Peter Piot anasema hali halisi kwa sasa ya ugonjwa huo ni kama ugonjwa utakaodumu muda mrefu.

Profesa Peter Piot ambaye amerejea kutoka nchini Sierra Leone, nchi ambayo imeathiriwa zaidi na ugonjwa huo, ameiambia BBC kwamba amehamasishwa na ahadi za kupatikana kwa kinga mpya ambayo inaaminika itakuwa tayari katika kipindi cha miezi mitatu.

Hata hivyo Profesa Piot ambaye aligundua virusi vya ugonjwa wa Ebola mwaka 1976, ameonya pia kwamba janga lililopo sasa halitakuwa la mwishon na chanjo kudhibiti kirusi hicho itachukua muda kufanya kazi