Amwacha mumewe na dadake uchi barabarani

Haki miliki ya picha Discovery Channel
Image caption Wawachwa uchi

Mwanamke kwa jina Ting Su nchini Uchina alimwacha mumewe na dadake bila nguo barabarani baada ya kuwapata wakifanya mapenzi Ting Ting Su aligundua kwamba mumewe alikuwa akimdanganya na dadaake na kuwafuata hadi katika kituo kimocha cha maduka akitumia teknologia katika simu yake ambapo aliwapata wakichemshana katika gari la mumewe.

Wawili hao walitoka ndani ya gari hilo bila nguo kwa kubabaika ili kujaribu kumuelezea kilichokuwa kikendelea lakini waliwachwa na mshangao mkubwa wakati Ting alipoingia ndani ya gari hilo na kuondoka kwa haraka na kuwawacha wawili hao barabarani bila nguo.

Kulingana na gazeti la Metro,shahidi aliyejulikana kama You Meng alisema walioshuhudia kisa hicho walibeba simu zao na kuanza kuchukua picha na yeye hakubakia nyuma.

Mumuwe aligonga dirisha la gari hilo na kumpigia kele mkewe lakini hakujali kamwe aliliondosha gari hilo kwa haraka.