B.Rodgers:Balotelli hawezi mtindo wetu

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption MKufunzi wa Liverpool Breand Rodgers asema baloteli haingiliani na mtindo wa liverpool

Mkufunzi wa Liverpool Brenda Rodgers amekiri kwamba mshambuliaji asiyefunga Mario baloteli haingiliani na mtindo wa kiufundi wa timu hiyo.

Balotteli mwenye umri wa miaka 24 amefunga mabao mawili katika mechi zote tangua ajiunge na kilabu hiyo kutoka AC Milan kwa pauni millioni 16 mnamo mwezi Agosti na Rodgers anaiwekea hatma ya mchezaji huyo atika njia panda.

Mchezaji huyo amekumbwa na utata kufikia sasa ,na tayari amehudumia marufuku ya mechi moja kufuatia maandishi alioandika katika mitandao ya kijamii ambayo yameonekana kuwa kinyume cha sheria za shirikisho la soka nchini Uingereza FA.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mario Balotelli

Huku timu hiyo ikikabiliwa na mechi ya Ugenini dhidi ya Burnley siku ya Boxing day,Rodgers alisema:''Nadhani tumegundua kuwa hawezi kucheza vizuri katika mtindo wa 3-4-4 tunaochezesha.

Tangu nifanye kazi na balotteli kwa kipindi ambacho amekuwa hapa,tumegundua kuwa ni mchezaji ambaye ni mzuri katika eneo la hatari kwa hivyo ile hali ya kutafuta si mchezo wake''..