Mtu aliyetabiri mwisho wa dunia afariki

Image caption Kiongozi wa kanisa la house of Yahweh nchini kenya aliyetabiri mwisho wa dunia mwaka 2006 afariki

Kiongozi mmoja wa dini ambaye alipata umaarufu nchini Kenya kwa kutabiri mwisho wa dunia mwaka 2006 amezikwa katika kijiji cha Bomet.

Kiongozi huyo wa madhehebu ya House of Yahweh Willy Kiplangat Sang alizikwa masaa machache baada ya kifo chake katika shamba la babaake kijijini Matarmat katika sherehe iliohudhuriwa na jamii yake ,majirani na wafuasi wa kanisa hilo.

Ndugu za nabii huyo aliyezingirwa na utata wanasema aliugua ugonjwa wa kifua kikuu nyumbani mwake huko Mauche kaunti ya Nakuru ambapo alikuwa mkulima na muhubiri.